Halloween Costume ideas 2015
Articles by "habari"


Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis yupo pamoja na jopu la viongozi wa kikatoliki duniani katika marekebisho ya sheria ya ndoa.

Katika marekebisho hayo pia inatarajiwa kuzungumzia urahishaji wa kipengele cha taraka katika ndoa kwa kuwa imekuwa ikiwabana watu wengi katika mazingira magumu.

Awali katika sheria ya ndoa kuhusu taraka iliidhinishwa toka kipindi cha Petro na Paulo ya kuwa hakuna ruhusa ya taraka katika ndoa kama jinsi alivyosema Nabii Yesu Kristo katika maandiko matakatifu ya Biblia, kwa hiyo taraka haitakiwi lakini kutokana na ugumu wa mioyo wa wanadamu wa sasa imekuwa ni vigumu kuepuka swala la taraka ambapo kwa sasa inatarajiwa kujadiliwa kwa kina uwezekano wa kurahisisha hapo kama ikiwa ndoa haikuwa halali.


Nchi ya ujerumani imeamua kuweka mkakati madhubuti wa kuweza kukabiliana na ongezeko la wahamiaji katika nchi hiyo.

Katika kuhakikisha kuwepo na hali nzuri katika nchi hiyo Ujerumani imetenga kiasi cha dola bilioni tatu kwa kuwekeza katika majimbo yake ili kuweza kukidhi mazingira bora ya raia wake pamoja na wageni ambao wataingia humo.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya nchi kadhaa za Ulaya kukubaliana katika mkakati wa kukabili ongezeko la uhamiaji barani humo ambao wengi wanatokea Afrika ya Magharibi pamoja Asia mara baada ya nchi zaoi kukumbwa na migogoro kadhaa ya kisiasa ambapo inatarajiwa wahamiaji elfu kumi na nane watakuwa wameingia nchini humo mapema.



Mahakama moja nchini Marekani imetoa hukumu ya jela kwa afisa mmoja wa serikali anyefahamika kwa jina la Kim Davies kwa kosa la kukataa kusaini cheti cha ndoa ya jnsia moja.




Maamuzi hayo yalitolewa na jaji katika mahakama hiyo mara baada ya Kim kugundurika kukataa kabisa kusaini cheti hicho kwa kuwa ndoa hiyo kwa kuwa inaenda tofauti na imani yake.



Ikumbukwe pia kuwa mwaka huu Marekani ilitangaza rasmi kuruhusu ndoa ya jinsia moja na kukataa kwa afisa huyo ni kukiuka kabisa sheria hiyo ambapo waumini mbalimbali wenye itikadi na imani tofauti wametoa mawazo yao kuhusuana na kitendo hicho huku baadhi wakimtuhum kwa kosa hilo na wengine wakimpongeza kwa ushujaa huo

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget