Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis yupo pamoja na jopu la viongozi wa kikatoliki duniani katika marekebisho ya sheria ya ndoa.
Katika marekebisho hayo pia inatarajiwa kuzungumzia urahishaji wa kipengele cha taraka katika ndoa kwa kuwa imekuwa ikiwabana watu wengi katika mazingira magumu.
Awali katika sheria ya ndoa kuhusu taraka iliidhinishwa toka kipindi cha Petro na Paulo ya kuwa hakuna ruhusa ya taraka katika ndoa kama jinsi alivyosema Nabii Yesu Kristo katika maandiko matakatifu ya Biblia, kwa hiyo taraka haitakiwi lakini kutokana na ugumu wa mioyo wa wanadamu wa sasa imekuwa ni vigumu kuepuka swala la taraka ambapo kwa sasa inatarajiwa kujadiliwa kwa kina uwezekano wa kurahisisha hapo kama ikiwa ndoa haikuwa halali.