Mgombea wa uraisi kupitia chama cha CCM mh.Magufuli amehaidi kuijenga tanzania mpya katika sura mpya pindi atakapochaguliwa katika uchaguzi mkuu oktoba. Katika maelezo yake mh.Magufuli ametambua vyema kazi zilizofanywa na maraisi waliopita na hivyo kuingia kwake madarakani pindi atakapochaguliwa ni kukamilsha kabisa kazi iliyojengwa na viongozi waliopita. Maelezo yake hayo yametolewa mara baada ya kupita sehem mbalimbali katika kunadi sera na mikakati ambayo kupitia chama cha CCM imepanga kutimiza pindi atakapochaguliwa kuwa raisi octoba mwaka huu katika uchaguzi mkuu.